Kuhusu maisha katika Dar

July 30th, 2009 by mohochi

Katelyn,

Nafurahi sana kusikia kuhusu maisha yako huko Dar. Aidha, nii vyema kuwa umeboresha Kiswahili chako. Hongera sana. Usemavyo, ni kweli kuwa maisha ya Dar ni mazuri. Nakutakia safari njema kwenda Moshi. Kila la heri katika harakati za kuukwea mlima Kilimanjaro. Natumai nitasikia maoni ya wengine kuhusu maisha na masomo yao huko Afrika Mashariki.