
Sasa nimesoma Kiswahili hapa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa wiki sita. Nitamaliza masomo yangu na Taaluma Institute kesho - Ijumaa, tarehe thelathini na moja, mwezi wa saba. Nilipenda sana kusoma Kiswahili hapa. Nilisoma na Mwalimu Mkuu Aldin Mutembei na Walimu Wadogo Happy na Nanci. Kiswahili yangu kimeboresha sana. Maisha katika Dar ni nzuri pia. Ni wakati wa kwanza kutembelea mji huu, na kweli, watu hapa ni wazuri sana. Naisha hapa kama Watanzania, kwa sababu kila asubuhi huamka saa mbili, na naenda darasani kwa daladala. Kutumia daladala kila siku ni kuishi kama Watanzania, nafikiri. Wanafunzi wa Taaluma wanakaa huko barabara Changanyikeni, katika Taakwim Hosteli, sehemu ya Chuo. Kwani nilifika, nimetembelea Mikumi National Park, mahali ambapo niliona simba kumi na mbili! Pia nimetembelea Kunduchi Beach, Kipepeo Beach na Malaika beach. Napenda sana kuogelea baharani kwa sababu hali ya hewa ni safi sana. Jumamosi iliopita, nilienda Bagamoyo peke yangu, ili kutembelea mahali ambapo palikuwa mji mkuu wa German Afrika ya Mashariki zamani. Huko, nilikutana watu wawili ambao walinialika kupika nao. Nilijifunza kupika chakula cha Watanzania - kama wali nazi, kabachi na vitunguu na nyanya, na maharagwe na mbogamboga. Nimefurahia sana kukaa hapa Dar es Salaam kwa wiki sita. Jumamoshi, tarehe moja, mwezi wa nane, naondoka kwa Moshi, ili kupanda Mlima Kilimanjaro na rafiki yangu Dan. Tutajaribu kufika juu ya Kili - Uhuru - pajoma. Itakuwa ngumu sana, lakini nitajitahidi! Sawa, baadaye.