Hawa ni Sarah na Jessica, na sisi tuko Nairobi. Jessica alifika wiki nne zilizopita, na Sarah alifika wiki mbili zilizopita. Tunakaa hapa Donholm, iko mashariki ya Nairobi. Tunaenda darasa la Kiswahili kila siku kwa saa tatu, na tunafanya “internships” na utafiti. Jessica ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Michigan State, na yeye anasoma “social work.” Atapata shahada ya uzamifu (PhD) katika mwaka 2012. Sarah alipata shahada ya kwanza kutoka chuo kikuu cha Stanford mwaka huu, na yeye angependa kutuma mombi katika masomo shahada ya pili wakati ujao. Tunasoma Kiswahili katika kiwango cha miaka wa pili, na tunapenda darasa la Kiswahili. Tulienda Maasai Market, Nairobi National Park, na mahali pingine hapa Nairobi. Tutatembelea Nakuru, Mombasa, Isebania, na Maasai Mara kabla ya kumaliza kusoma.
Nini ni nani, na mnafanya nini? Habari za Dar es Salaam?